Artists News in Tanzania

Mr. Nice Alitumwa na Mungu – Wabogojo

Msanii Mtanzania ambaye anafanya shughuli zake nchini Macau Othman Ford (Wabogojo) amesema anamuheshimu sana Mr. Nice kwani alitumwa na Mungu kuja kumtoa yeye kisanaa.

Wabogojo amesema Mr. Nice ndiye alimtoa kwenye na kumfanya kuanza kujulikana kwa watu, hivyo kwake ni sawa na bosi wake na kila akirudi hapa nchini lazima aende nyumbani kwake kujua anaendeleaje na shughuli zake.

“Mr. Nice ndio bosi wangu, Mr. Nice ndio ambaye alifanya Watanzania, Wakenya, Wauganda na mataifa mbali mbali wakanitambua mimi, Mwenyezi Mungu alimtumia Mr. Nice kuninyanyua mimi, hata kama labda sijapata pesa nyingi sana kipindi niko na Mr. Nice lakini kitu nilichokipata kutoka kwa Mr. Nice ni zaidi ya fedha hata mi mwenyewe namwambiaga, ndio maana mpaka sasa hivi yule jamaa namuheshimu, kila nikirudi lazima niwasiliane nae na naendaga mpaka kwao”, alisema Wabogojo ambaye pia ni kaka wa msanii wa bongo movies Shamsa Ford.

Pamoja na hayo akielezea changamoto ya kufanya sanaa nje ya nchi yake, wabogojo amesema alikuwa anapata shida siku za mwanzoni kutokana na lugha ya Kiswahili aliyokuwa akitumia, kushindwa kuwasiliana na watu wa jamii ya huko.

“Changamoto kubwa ilikuwa, lugha sisi ni waswahili hata shule hatutumii english, unaenda supermarket kununua lotion unanunua sabuni, tulikuwa tunajifunza pia kuishi mazingiraya kule”, alisema Wabogojo.

Comments

comments

Exit mobile version