Kupitia Ukurasa wake kwenye mtandao wa instagram, muigizaji Fredy Swai aliyetajwa na mama mzazi wa marehemu Kanumba kuwa ndiye mrithi atakae vaa viatu vya mtoto wake , Kanumba katika tasnia ya uigizaji , amefunga haya mara baada ya kuweka picha ya Kanumba;
Haimaanishi kwamba uliimaliza sanaa yote iliyoandikwa kwenye vitabu.. Ila kwa hapa Tanzania ulipokua umefikia ni mbali sana.. Ni miaka mitano lakini hakuna aliyefika ulipopaacha.. UKWELI NI KWAMBA #kilabinadamu anakitu chake alichopewa na Mungu ndo maana ni ngumu kufanana nafsi labda kuiga tuu.. Ila kama KILA BINADAMU anavitu vyake bas WACHA NASISI TUFANYE VYETU na zaidi haswa ni kufanya vikubwa zaidi..! Siwez kusema ulale mahali pema kwa vile MUNGU TU ndiye anayepanga pakukupeleka ww na kwa neno langu siwez kukupangia pakwenda… Ila tunakukumbuka na tutakukumbuka pia haswa kwa hatua uliyofikia.
Kwasasa Fredy anatamba kwenye tamthilia ya DHAMIRA.
Comments
comments