Msanii Akiri Kuwahi Kwenda kwa Mganga
Msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Samaki’ Galatone amefunguka na kusema kuwa yeye aliwahi kwenda kwa mganga wa kienyeji kufanya makeke ili aone jambo ambalo linamsumbua.
Galatone alisema hayo kupitia kipindi cha ‘NgazKwaNgaz’ kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana EATV, msanii huyo anasema katika hali ya kawaida kuna mambo yanaweza kukutokea na kukufanya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili kujua tatizo.
“Yah kwa mganga mimi nimeshawahi kwenda, unajua katika maisha ya kila siku tunayoishi kibinadamu kuna vitu vingine vinaweza kukutokea ukahisi hiki kitu ni cha tofauti na si cha kawaida. Kwa mfano umelala vizuri msafi halafu unaamka asubuhi unajikuta una matope mwili mzima hivyo hicho hakikufanyi uende kwa mganga kweli? Kitu hiki kinaweza kukufanya ukaingia kwenye imani ukawaambia jamanii eehh niangalizieni hiki kitu” alisema Galatone
Mbali na hilo Galatone anasema kipindi anasoma anakumbuka maisha yalikuwa taiti na pesa anazopewa zilikuwa hazitoshi kwa matumizi yake hivyo alikuwa mwizi sana wa vitu vya watu kiasi cha wanafunzi wote hostel walikuwa wanajua kuwa jamaa ni mpigaji kwa vitu vya shule kama Blue band, misosi n.k.