Mtanzania Ahukumiwa Jela Miezi 3 Uingereza, Kisa Kuweka Post Hii Facebook
Mwanaume mmoja mwenye asili ya kitanzania, Omega Mwaikambo (43) amekamatwa nchini Uingereza kwa kosa la kuweka picha za mwili wa mtu aliyefariki katika ajali ya moto kwenye mtandao wa Facebook.
Mwaikambo ameukumiwa kifungo cha miezi miatatu jela pamoja na kulipa faini ya kwenda jela miezi 3 kwa kosa hilo huku akitakiwa pia kulipa faini ya shilingi 579,880 kwa familia ya marehemu huyo.
Licha ya kukiri kufanya kosa hilo mbele ya hakimu wa mahakama ya Westerminister jana, mwanaume huyo amejitete kwa kueleza kuwa aliweka picha hizo mbili katika mtandao huo wa jamii ilikurahisisha utambuzi wa mwili wa marehemu.
Kwa mujibu wa gazeti la The Teleghraph la Uingereza limesema, Omega aliweka picha hizo mbili katika Facebook yake kwa kutumia simu yake ya Ipad ni baada ya kutoka nje ya nyumba yake na kukuta miili hiyo.
Hata hivyo mwendesha mashtaka katika mahakama hiyo, Tanweer Ikram amesema kuwa kitendo likichofanywa na mtu huyo siku ya Jumatano si kizuri kwani maiti lazima iheshimiwe.
Bongo5