Mtitu Afunguka Maprodyuza Kuwamaliza Warembo
PRODYUZA na muigizaji wa sinema Bongo, William Mtitu amefunguka kuwa maprodyuza wengi wamekuwa wakipewa lawama za kutembea na waigizaji wa kike kutokana na wao wenyewe kujirahisisha.
Akizungumza na mwanahabari wetu ofisini kwake Magomeni jijini Dar, Mtitu alisema endapo warembo wenyewe wakijitambua, hakutakuwa na malalamiko hayo kila kukicha.
“Wanajirahisisha wenyewe halafu baadaye wanalalamika katika vyombo vya habari, binafsi huwa nawapuuza hata wakijirahisisha lakini kwa kuwa nafanya nao kazi, nawajua. Wabadilike waone kama tatizo litaendelea,” alisema Mtitu.
Chanzo:GPL