-->

Mtitu Akumbuka Enzi na ‘Mama Mkubwa’ Ndani ya ITV!

MUONGOZAJI wa filamu na mkurugenzi wa 5 Effect William Mtitu ‘Mtitu’  ameamua kurudi kwenye tamthilia na kuipa nguvu zaidi tofauti na filamu, Mtitu anasema misingi imara inapatikana kwa wasanii waliopitia katika tamthilia na kuingia katika filamu.

mama-mkubwa-34

“Nilikuwa nikifanya utafiti nakugundua kuwa tamthilia imetoa vipaji vingi sana, nami nimeona bora nijikite huko na tumefanikiwa kuja na tamthilia kubwa sana ya Mama Kubwa, itakayoteka nyoyo za wapenzi wa maigizo,”

Mtitu mtayarishaji na muongozaji wa Mama Mkubwa

Mtitu mtayarishaji na muongozaji wa Mama Mkubwa

Mtitu anasema kuwa tamthilia hiyo itarushwa katika kituo cha ITV kila siku ya jumapili imewashirikisha wasanii kama Zebwe Mrisho, Alex Wasponga ‘Baba James’, Mariam Ismail, Getrude Mwita, na wasanii wengi wanaotamba katika tasnia ya filamu Swahilihood na imeongozwa na Mtitu .

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364