-->

Mtunis: Filamu za Bongo Zinalipa Sana

STAA wa filamu nchini, Nice Mohammed ‘Mtunis’, alisema soko la filamu litakuwa kubwa kama filamu zinazozalishwa nchini zitakuwa na ubora unaotakiwa kwa jamii ambao ndio wanunuaji.

MTUNIS

Mtunis aliliambia MTANZANIA kwamba licha ya waigizaji na wadau wengi kudai kwamba filamu za Bongo hazilipi yeye anasema kwamba filamu hizo zinalipa ila zisizolipa ni zile zinazokosa uandaaji mzuri.

“Kujikosoa ndiyo dawa, hayo mengine tunatapatapa, filamu nzuri na zenye viwango zinalipa na baadhi ya filamu nzuri zipo nchini lakini wengi hatutaki kukubali ukweli huo ndiyo maana wengi wetu wanabaki kudanganya kwamba filamu hazilipi wakati tunaofanya vizuri tunaingiza fedha za kutosha,” alisema Mtunis.

Mtunis aliongeza kwamba filamu bora ikijengewa misingi bora na kuchezwa kwa kuangalia misingi ya uigizaji huku hadithi yake ikiwa na mvuto na elimu kwa jamii itaongeza imani kwa mashabiki na wadau wa filamu.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364