-->

Mubenga: Nimepata Mbadala wa Ommy Dimpoz!!

TOFAUTI kati ya mafahari wawili, staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na aliyewahi kuwa meneja wake, Mbarouk Ogga ‘Mubenga’ zinazidi kuchukua sura mpya baada ya hivi karibuni Mubenga ambaye kwa sasa anamiliki kampuni iitwayo Bengaz Entertainment kuibuka na kudai amempata mbadala wa Dimpoz.

ommy-na-mubenga

Ommy Dimpoz na Mubenga

Mubenga na Dimpoz waliingia kwenye tofauti zilizosababisha mpaka meneja huyo kujitoa kwenye kampuni ya Dimpoz iitwayo Pozi Kwa Pozi kwa madai kuwa Dimpoz aliweka bondi gari lake na kudaiwa dola elfu kumi ambazo ni sawa na shilingi milioni 21 za Kitanzania bila yeye kufahamu.

Hata hivyo, akichonga na Risasi BMM, kuhusu suala hilo Mubenga alifunguka kuwa kikubwa kilichomtoa PKP ni masilahi. Kwamba hakuwa anapata masilahi yoyote zaidi ya kupiga kazi na Dimpoz huku akimchukulia kama ndugu yake kutokana na kutoka naye kwenye sifuri mpaka kufikia hatua hiyo ya Dimpoz kupata mafanikio na kufahamika kila sehemu. Hebu msikie;

“Siwezi kusema mengi au kuzungumzia masuala ambayo yana ‘trend’ kwenye mitandao ya kijamii na media mbalimbali, kikubwa kilichonitoa PKP hakuna mafanikio niliyokuwa nayapata.

“Mbaya zaidi ilifika hatua Dimpoz ambaye kabla ya kufika hapo alipo alikuwa ananisikiliza na tunapanga pamoja ni vipi tufanye kazi, lakini ilifika hatua akawa hasikii lolote lile kutoka kwangu. Mafanikio yalimlewesha akasahau alipotoka, sasa, mimi nimeamua kumuacha na nimepata mbadala wake ambaye nina uhakika nitafika naye mbali,” amesema Mubenga.

Akimzungumzia msanii huyo mbadala wa Dimpoz, Mubenga anaendelea kufunguka kuwa, jamaa anaitwa Moses Njenga ‘MossRed’. Mbongo anayeishi Sauz na huko ndiko alikoanza harakati za muziki na anafahamika zaidi kuliko Bongo.

“Mashabiki wa Bongo wanaweza kuwa hawamfahamu Mossred. Lakini wasanii wengi wanamfahamu kwa sababu amewasaidia unaowaona wamefanyia kazi Sauz, iwe kushuti au kurekodi, wengi huwa wanafikia katika mikono yake.

“MossRed pia ndiye msanii wa mwisho kufanya kazi na Albert Mangwea maana walirekodi jioni na usiku mshikaji akapoteza maisha. Ni yeye pia aliyekuwa amemkatia tiketi ya kurudi Bongo.”

Mubenga amefunguka mengi sana kuhusu MossRed aliyeanza gemu mwaka 2010 akiwa Sauz na anamiliki studio nchini humo na Kundi liitwalo Feza Gang One.

Kuhusu kazi mpaka sasa Mossred anayerap Kiswahili na Kiingereza amefanikiwa kufanya ‘mixtape’ nne ambazo zinaitwa Mwanzo vol. 1, Mwanzo vol. 2. Mwanzo vol. 3 na Mwanzo vol 4, lakini pia amewahi kupiga kolabo na Ali Kiba, ngoma inaitwa The Way You Shine.

Kwa upande wa MossRed akizungumzia kuhusu kupiga mzigo Bongo akiwa na Bengaz Entertainment amesema anafurahi sana na anauhakika wa kufanya vizuri ukanda wa Afrika Mashariki kwa sababu amekwishalisoma gemu la Bongo na zaidi yeye amepiga hatua moja ya kukubalika Afrika Magharibi.

“Kikubwa naomba Wabongo wanisapoti katika kazi zangu na ninafurahi sana kufanya kazi na Mubenga, nina uhakika tutafanya makubwa kwenye tasnia kwa sababu ni mtu anayefahamu namna ya kumsimamia msanii,” anamaliza MossRed.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364