Artists News in Tanzania

Mwakyembe Apiga Marufuku Tuzo za Muziki na Mashindano ya Miss Tanzania

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku uandaaji na uendeshwaji wa mashindano ya urembo (Miss Tanzania) na tuzo za muziki hapa nchini kutokana na ubabaishaji wa waandaaji wa mashindano hayo.
Mwakyembe amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji wa hali ya juu ambapo kwenye utoaji wa tuzo kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuwapa washindi zawadi wanazoahidiwa jambo linaloleta usumbufu na mitafaruku.
Ameongeza kuwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo ni lazima zawadi wanazoahidi kuwapa washindi zipelekwe ofisini kwa waziri huyo.
”Kwa sasa tutanakaa chini na wadau wa burudani juu ya mashindano hayo, lakini tunataka tuzo ziwe na (guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika na sio kufanyika kwa kubahatisha tu!”, alisema Mwakyembe.
Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version