Mwanamke lazima uwe na nyama-Shilole
staa mrembo wa bongo m ovie na bongo fleva, Shilole amefunguka kwa kusema kuwa mwanamke lakina uwe na maumbile manene ili kumvutia mwanaume.
Shilole ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kigori’, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa siyo sifa mbaya kunenepa hasa kwa mwanamke na kitu ambacho anajivunia.
“Mwanamke lazima uwe na sehemu mwanaume akikushika unashikika, mwanamke lazima uwe na nyama. Hatuwezi kuwa wote wembamba tutafanyaje kwenye industry hata Ulaya kuna wanene, siunaona sasa hivi Rihanna kanenepa lakini before alikuwa mwembamba alishaona upuuzi,” amesema Shilole.
Hata hivyo muimbaji huyo ameongeza kuwa mwili wake umekuja wenyewe wala hakuna jitihada zozote zilizofanyika kupelekea hali hiyo.