Artists News in Tanzania

Mwanaume wa Hivi Hafai Kabisa – Shamsa Ford

Msanii wa filamu nchini na mfanyabiashara Shamsa Ford amefunguka na kutoa somo kwa baadhi ya wanawake kuwa wakiona wapo kwenye mahusiano na mwanaume ambaye hajivunii uwepo wa mwanamke basi wajue wazi mtu huyo si wake bali atakuwa wa mtu mwingine.

Shamsa Ford

Shamsa Ford anasema mara nyingi wanawake wanapenda kuwa na mwanaume ambaye ana heshima na mapenzi ya dhati lakini pia mtu ambaye anajitoa kwa mpenzi wake kwa lolote pasipokuwa na wasiwasi wowote.

“Wanawake siku zote huwa tunapenda heshima, kupendwa, kuthaminiwa na kupewa kipaumbele na wanaume zetu. Mwanamke mwenzangu ukiona mwanaume haeleweki, hakuthamini, mapenzi mpaka muwe wawili ndiyo anakuonesha ila mbele za watu anazuga kama yupo na bibi yake basi ujue huyo si wako. Mwanaume anayekupenda na kukuthamini atatamani dunia nzima ijue kama anakupenda. Atakupenda na kukuthamini muda wowote bila kikwazo” Aliandika Shamsa Ford 

Shamsa Ford ni mke wa mfanyabiashara Chid Mapenzi ambaye naye ametajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika sakata la dawa za kulevya.

 

Comments

comments

Exit mobile version