Mzee Kambi Kuachia Filamu ‘Dar to Washington DC’ Iliyoandaliwa Marekani
Msanii wa filamu, Hashim Kambi amesema filamu yake mpya ‘Dar to Washington DC’ ambayo ilikuwa ikiandaliwa nchini Marekani huku ikishirikisha wasanii wa Tanzania na Marekani imekamilika.
Mwigizaji huyo ambaye bado jupo nchini Marekani, ameuambia mtandao wa Filamucentral kuwa, yupo mbioni kurudi Dar baada ya kukamilisha kazi hiyo.
“Ni zaidi ya mwezi mmoja sasa tumemaliza kushoot filamu yetu, lakini tupo katika mapumziko kwa sababu kuna baridi kali sana kwa sasa. Tunatumia muda huu kuweza kutembelea sehemu mbalimbali,” alisema Mzee Kambi.
Dar to Washington DC imechezwa na Hashim Kambi ‘Ramsey’, Charles Magali ‘Mzee Magali’ Mohamed Mwikongi ‘Frank’ na wasanii wengine kutoka Marekani.
Bongo5