Muigizaji wa filamu nchini mzee Majuto amefunguka na kusema kuwa mwaka 2017 amepanga kufanya mambo matatu ambayo yote anataka yaende pamoja.
Jambo la kwanza ni kuhusiana na sanaa yake ambapo amepanga kwa mwaka huu wa 2017 kuhakikisha kazi zake za sanaa anazisambaza mwenyewe na kuachana na wasambazaji wengine.
Mzee Majuto amesema jambo la pili katika mwaka huu ambalo pia atalifanya sana ni kuhakikisha ana mcha Mungu sana na jambo la mwisho ni kufanya kilimo na ufugaji ili kijiongezea kipato chake.
“Mwaka huu nimepanga mambo matatu kwanza kumcha Mungu sana, kuigiza kama kawaida na mwaka huu nataka kazi zangu nizisimamie mweyewe kusambaza na kuachana na wasambazaji wengine katika kazi zangu lakini jambo lingine kulima na kufanya ufugaji, maana saizi nimejiunga na mtandao wa kijani, nafuga Sungura, nalima mchai chai” alisema Mzee Majuto
eatv.tv
Comments
comments