Mzee Majuto Awapa Changamoto Hii Bongo Movie
Msanii mkongwe wa filamu Bongo, King Majuto amewataka wasanii ambao wapo katika tasnia hiyo kufanya kazi zenye ubora ili kufikia mafanikio kama yake.
Muigizaji huyu ambaye alitangaza kustaafu kuigiza ameiambia Azam Tv kuwa kwa sasa hivi wasanii wanapendwa na serikili inawatambua hivyo watumie fursa hiyo kufanya kazi.
“Kwa hiyo msichoke, fanyeni jitihada, tengenezeni michezo yenye busara, tengenezeni michezo inayoeleweka msifanye ilimradi tu na heshimuni bodi ya filamu ili mfanye kazi nzuri” amesema King Majuto.
Bongo5