Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kumpa sifa mzazi mwenzake Chuchu Hansy ambaye leo alikuwa anasherekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kuwa bado ni mbichi licha ya kujifungua siku za karibuni.
Ray Kigosi amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema licha ya mrembo wake huyo kujifungua lakini hajabadilika kama ambavyo huenda alikuwa akidhani labda akipata mtoto anaweza kuharibika na kupoteza muonekano wake.
“Mzungu wangu bado mbichi utafikiri ujajifungua juzi kweli kujifungua siyo kuzeeka ‘Happy birthday to you mama Jaden Chuchu Hans” aliandika Ray Kigosi
Aidha Ray Kigosi ametumia siku hiyo ya kuzaliwa kwa mzazi mwenzake kumshukuru kwa kuweza kumpa heshima na kumbadili jina na sasa kuitwa baba
“Asante sana kwa kuwa mama bora kabisa kwa mwenetu Jaden hakika hakuna wa kufanana na wewe nina mengi sana ya kukwambia ila wacha leo kwenye siku yako ya kuzaliwa nikwambie haya machache nakupenda, nakuthamini na kukujali. Pia nitakuwa nafanya kosa kubwa kama sitomshukuru Mungu kwa kunizalia mtoto mzuri na kunipa heshima kubwa ya kuitwa baba” aliandika Ray Kigosi
Comments
comments