Baada kuibuka maswali mengi kuhusu picha ambazo zilikuwa zikirushwa katika mitandao ya kijamii kuhusu kuvalishwa kwa Pete ya uchumba kwa msanii mahiri wa Filamu na tamthilia Bongo Coletha Raymond ‘Koleta’ si Filamu ni kweli akiongea na FC msanii huyo huku akicheka alisema kufuatia picha hizo watu wanaompigia simu wameongezeka wakitaka kujua kama ni yeye.
“Wasanii tunachangamoto kubwa sana katika masuala ya ndoa kwani hata pale inapotokea jambo la kweli bado watu wanahisi ni kuigiza kila mtu aliyenipigia simu alitaka kujua kama mimi kweli na kuna wale waliojua kuwa nipo Location nikiigiza kama ilivyozoeleka kwetu wasanii”, alisema Korea.
Aidha Koleta amesema kuwa kufuatia picha zake kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kwake kwani kila anayeongea naye akitaka kujua kama tukio hilo ni kweli na yeye ana tumia mwanya huo kuomba michango ya kufanikisha harusi yake ambayo anaamini kuwa itakuwa harusi ya kihistoria kufungwa na msanii mkubwa na mkongwe nchini kwani pia ni hamasa kwa wasanii wenzake wenye mawazo kuwa ndoa lazima wawe na mamilioni ya fedha.
Asilimia kubwa ya wasanii Nyota Swahilihood hawapo katika maisha ya ndoa huku zile ambazo ziliwahi kufungwa gharama kubwa zikiwa kwenye sintofahamu huku wengine wakiwa wamefanikiwa kuzaa au kuwazalisha wanawake ambao hawapo nao huku maisha na wao wakiishi pekee yao.
Katika kutafuta ukweli wa jambo hilo ambalo limetaaliwa na hofu kwa wapenzi wa Filamu Bongo mwandishi alimpata mmoja ya wasanii walioshuhudia tukio hilo la kuvalishwa Pete Koleta ambaye ni Salum Mchoma almaarufu kama Teacher Chiki alikiri kuwa ni tukio la kweli na wapo katika harakati za kuandaa vikao kwa ajili sherehe za kuandaa sherehe za kumuaga msanii mwezao.
“Hiyo si sinema ni tukio halisi kiongozi si sinema Koleta kapata mwezake hivyo tupo katika mipango ya kuandaa Sendoff na nimeamua kuchukua nafasi ya kulisimamia jambo hili kwa nguvu sana maana wasanii hawataki kuoa kwa woga wa gharama,”alisema Chiki.
Koleta amedai kuwa sherehe za kuagwa (Sendoff party) ambayo inatarajia kufanyika tarehe 23. February. 2017 na harusi inatarajia kufungwa tarehe 25. February. 2017 Dar Es Salaam.
Comments
comments