Napenda kufanya movie za mapenzi kama Kanumba – Tunda
Video vixen Bongo, Tunda amefunguka mipango yake ya kutaka kuingia katika uigizaji wa movie.
Tunda amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula hasa katika upande wa movie za mapenzi.
“Kila kitu kina process ikifika kama inaruhusu nitafanya, napenda kufanya za mapenzi kama za Kanumba” Tunda ameiambia Bongo5.
Katika hatua nyingine Tunda amesema si kweli alitoa/umetoka ujauzito wake bali ni kitu ambacho hakuwa nacho kabisa bali kunenepa kwake ndipo kuliko changia watu kuhisi hivyo.