“Narudisha Status Yangu Sasa” – Nuhu Mziwanda
Msanii Nuh Mziwanda amesema hajutii maisha yake aliyoyapitia akiwa na mpenzi wake wa zamani, kwani amesha move on (kusonga mbele).
Nuhu Mziwanda ambaye hivi karibuni ameachia kazi yake ya ‘Jike Shupa’ aliyomshirikisha Ali Kiba, ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha 5SELEKT cha EATV, na kusema kuwa kwa sasa yeye anachofikiria ni kazi zaidi.
“Kujuta kupo lakini sijuti kwa sababu nishaendelea, nimesha move on (songa mbele ) na maisha yangu na nafanya kazi zangu,” alisema Nuhu Mziwanda.
Pia Nuhu Mziwanda amezungumzia mahusiano yake ya sasa ambaye amekiri kufahamiana na mwandani wake huyo kwenye mitandao ya kijamii, na kusema hataki tena maisha ya mitandaoni kwani alishayapitia, na anachokifanya kwa sasa ni kubadili status (hadhi) ya maisha yake.
“Sitaki kuweka mahusiano kwenye media (vyombo vya habari), sawa ni vizuri ukiamua kuweka wazi, nishapitia sana hayo maisha, nataka kurudisha status yangu, nimekaa kimya muda nimegundua nina mashabiki wengi, sitaki maisha ya skendo, sitaki status ya skendo,” alisema Nuhu Mziwanda.
eatv.tv