Nataka nifikishe watoto wanne – Flora Mvungi
Msanii wa filamu Flora Mvungi ambaye pia ni mke wa mwanamuziki H.Baba, amejibu shutuma zinazoongelewa na watu katika mitandao ya kijamii kuwa anazaa haraka haraka mno ambayo ni hatari kwa afya yake.
Akizungumza katika kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm, Flora amesema kila mtu ana maamuzi yake kuhusu maswala ya uzazi.
“Nataka nifikishe watoto wanne, kwa hiyo sasa hivi naenda kupata watatu, nahitaji nikianza kuigiza niwe free zaidi sitakuwa na majukumu ya uzazi tena,” alisema Flora.
Pia Flora amedai tangu aanze kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi mpaka leo hajawahi kujaribu wala kutumia uzazi wa Mpango.
H.Baba na Flora wamejaaliwa kupata watoto wawili, Tanzanite na Africa huku wakitegemea kupata mtoto wa tatu hivi karibuni.
Chanzo: Bongo5