Rapa Nay wa Mitego anayetamba na wimbo wa ‘Wapo’ uliojipatia umaarufu mkubwa hadi serikalini amedai kuwa usalama wa maisha yake upo hatarini na kwamba kuna watu wanaopanga kumpoteza ili asiwepo duniani.
Katika ukurasa wake wa Instagram Nay ‘amerusha jiwe gizani’ pasipo kumtaja mtu ambaye anataka kumuangamiza huku akisisistiza kuwa yupo tayari kufanyiwa chochote na kwamba hajajipanga kupambana na watu wao.
“Usalama wa maisha yangu umekuwa mdogo kwasasa, wanapanga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya coz sijajipanga kupambana nao” Ameandika Nay.
Nay ameongeza “Mimi ni Mwanamuziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea familia yangu itakuwa na cha kuongea. Siwezi kuhama nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina mlinzi na sitarajii kuwa na mlinzi. OnlyGod”
Nay ametoa taarifa hizo ikiwa ni siku chache baada ya kuachia wimbo huo na kukamatwa na polisi lakini baadaye akaachiwa kwa amri ya Rais na kujipatia nafasi ya kuonana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Comments
comments