RAPA mahiri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema endapo kitendo alichokifanya Ommy Dimpoz cha kuweka picha ya mzazi wa Diamond Platnumz kwenye Instagram yake, angefanyiwa yeye basi pangechimbika.
Mitego anayefanya poa na wimbo wake mpya, ‘Makuzi’ ameliambia ShowBiz kuwa anampenda sana mama yake mzazi hivyo adui anaweza kumtukana yeye au watoto wake kadiri awezavyo lakini asimtukane mama yake mzazi.
“Ilinibidi niandike yale maneno ya kuwaonya kwa sababu nampenda mama yangu, unajua unaweza kupata laana kwa kumtukana mwanamke yeyote yule mwenye uchungu wa kuzaa siyo lazima awe mama yako,” alisena Nay wa Mitego.
Comments
comments