Nay wa Mitego ni Mtoto Mdogo Kwangu Kisanaa- Niva
ZUBERY Mohamed ndio jina lake alilopewa na wazazi wake lakini katika filamu anajulikana kama Niva super Mario msanii huyu ambaye ni mwigizaji na mwanamuziki wa kizazi kipya anaibua malumbano na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ney wa Mitego na kusema kuwa ni mdogo katika sanaa.
“Unajua kwa wale wasiomjua Ney wa Mitego ndio wanamhofia lakini kwangu ni mtoto mdogo sana kisanaa mimi naimba naigizaji, malipo ninayomlipa msanii mmoja katika filamu yeye ndio anarekodia albamu haniwezi,”anasema Niva.
Malumbano ya wasanii hawa yaliibuka baada ya Ney wa Mitego kumuimba Niva katika moja ya wimbo wake akidai kuwa msanii huyo anaishi kwa kutegemea wanawake jambo linalomfanya asiweze kumiliki chumba jambo ambalo Niva anakanusha na kusema ni njia ya kutafuta kiki za kimuziki.
Wasanii wengi hususani wa filamu wamekuwa na wakati mgumu kutoka msanii huyo wa Bongo fleva kwa kutunga nyimbo zinazogusa maisha yao katika njia hasi, Niva anasisitiza kuwa Ney anataka kiki kupitia kwake huku Ney akidai kwa anachosema ni kweli.
FC