-->

Nay wa Mitego: Ya Barakah na Stan Bakora inaweza kuwa ni kiki

Nay wa Mitego amedai kuwa kinachoendelea kati ya Barakah The Prince na Stan Bakora, kinaweza kuwa kitu cha kutengeneza.

baraka45

Akiongea na mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove, rapper huyo amewaita wawili hao wote watoto na kwamba umri wao unawaruhusu kufanya wwanachokifanya.

“Siwezi kusimama upande wowote, hao ni watoto, wote ni wadogo mimi ni wadogo zangu,” alisema.

“So inapofika time wanagombana wataelewana tu. Hatuwezi kujua labda ni kiki, haiwezi kuwa beef kiasi hicho, inawezekana labda kiki, watu mkachukulia serious kumbe wamekaa wametengeneza,” ameongeza Nay.

Barakah ameonekana kuchukizwa na parody aliyofanya Stan ya wimbo wake Nisamehe ambapo amejipaka masizi usoni kuwa mweusi kama muimbaji huyo.

Stan amejipatia umaarufu kwa kuigiza sauti ya Nay wa Mitego.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364