Artists News in Tanzania

Nikikutana na Nay wa Mitego sina time naye, Tunapishana Tu – Shamsa Ford

Shamsa Ford na Nay wa Mitego ni pua na moshi. Shamsa Ford amesema akikutana na Nay wa Mitego hawezi salimiana naye kutokana na mambo ambayo walifanyiana.

Mwigizaji huo wa filamu aliwahi kukiri kwamba hawezi toka tena kimapenzi na staa, ikiwa ni muda mchache toka aachane na Nay wa Mitego.

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Shamsa alisema Nay sio mshikaji wake tena na yaliyotokea kati yao anayachukulia kama ni sehemu ya maisha ambayo alitakiwa kuyapitia ili ajifunze.

“Hukana mkorofi tuliamua tu mahusiano yetu yafike mwisho. Hamna tena ushikaji tena wala ‘ucousin’ ulishaisha kila mtu ana maisha yake, tukionana vikumbo tu,” alisema Shamsa.

Katika hatua nyingine Shamsa amewatakama mashabiki wa filamu zake kuifuatilia filamu yake mpya iitwayo ‘Najuta Shamsa’.

Chanzo: Bongo 5

Comments

comments

Exit mobile version