Msanii Nikki wa Pili amepingana na kauli ya msanii mwenzake wa hip hop rapa Baghdad aliposema kutopendana kwa wasanii hao kutasababisha muziki wa hip hop bongo kufa.
Akizungumza na EATV Nikki wa Pili amesema ingawa kutopendana kwa wasanii kupo kutokana na kazi wanayofanya kuwa ya ushindani, muziki wa hip hop hauwezi kufa kwani hiyo siyo sababu hata kidogo ya kuua hip hop ya Bongo.
“Kwenye ushindani watu wowote wanaouza bidhaa inayofanana hawawezi kupendana kivile kwa sababu wale ni competitor, lakini ukisema wasanii wa hip hop hawapendani sielewi, wasanii wa hip hop wanashirikiana, wana collabo nyingi sana baina ya wasanii na wasanii, na mimi siamini kama hip hop inaweza ikafa kwa kupendana au kwa kuchukiana, kitakachofanya muziki ukue ni juhudi za kila msanii, na kitakachokuja kufanya muziki urudi nyuma ni kila msanii moja mmoja kutokuwa na juhudi”, alisema Nikki wa Pili.
Hivi juzi rapa Baghdaa alisikika kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio akisema hip hop ya bongo ipo katika hatari ya kufa kutokana na chuki iliyopo kati ya wasanii wa muziki huo wa bongo.
eatv.tv
Comments
comments