Artists News in Tanzania

Nikki : Wasomi Acheni Kulia Kulia

Rapa msomi kutoka Weusi Kampuni, Nikki wa Pili amewataka wahitimu waache kulia na kulalamikia serikali kwa kukosa ajira na badala yake wanapaswa watumie uthubutu wao katika yale waliyojifunza darasani.

Nikki wa Pili

Nikki amefunguka hayo leo kupitia kipindi cha Supamix cha East Africa Radio baada ya wanafunzi wengi kutoka maeneno mbalimbali ya nchi wakionekena kukata tamaa ya maisha kwa kile kinachodiwa ukosefu wa ajira mara tu wanapohitimu masomo yao.

“Katika maisha ya sasa kuna uhakika wa kupata elimu na vilevile kufa masikini kwa sababu hakuna uthubutu kwa wanafunzi kutokana shuleni, wanasifu sana akili kuliko uthubutu. Watu wanaobadilisha dunia ni wale wenye uthubutu na siyo wenye akili za darasani” alisema Nikki wa pili.

Pamoja na hayo, Nikki ameendelea kwa kusema “Watu wenye diploma (Astashada) na wenye degree (shahada) ndiyo wanaongoza kwa kulalamika hakuna ajira huku waliomaliza darasa la saba wanapambana katika kutafuta pesa na wanafanikiwa kupata hela nyingi kuliko watu walioajiriwa.

Kwa upande mwingine Nikki amewashauri vijana waliyopo vyuoni wajitahidi kujifunza vitu vya nje ya darasani ili watakapofanikiwa kumaliza miaka yao mitatu basi wawe na maarifa mengine ya ziada.

EATV.TV

Comments

comments

Exit mobile version