Lile sakata la KR Mullah akiwa anaonekana kwenye picha, amelewa pombe chakari na msanii Juma Nature akaoneshwa kuguswa na tukio hilo, eNewz iliwatafuta wote wawili kila mmoja kwa wakati wake na kuzungumza nao.
Juma Nature ambaye alikuwa msanii wa kwanza kutuma picha zile kwenye ukurasa wake wa Instagram, amefunguka kwa kusema kuwa alitumiwa picha zile na kuambiwa amsaidie ndugu yake ambaye ni KR Mullah.
“Zile picha mimi nimetumiwa nikaambiwa mwangalie ndugu yako, japo alinisema vibaya lakini nilimtumia gari watu wamfate wampeleke ghetto kwake ila niliwahi kumwambia aangalie aende kufanya kazi na awe makini katika kazi zake” Amesema Juma Nature.
Nature aliongeza kwa kusema “Alichokunywa zile siyo pombe bali ni sembee mtu huwezi kunywa bia hivyo hadi ukalale kwenye mtaro kuanzia asubuhi mpaka saa 6” na pia Nature alimaliza kwa kusema akirudi TMK atampokea kwa sababu bado anampenda kama ndugu yake na milango iko wazi.
eNewz ilitaka kujiridhisha kwa kumtafuta KR Mullah na kuzungumza naye. Je, ni kweli Juma Nature alijitolea kumsaidia?
Alijibu kwa kusema kama angekuwa anamsaidia basi asingeweza kwenda kulalama kwenye mitandao ya kijamii. “Nasikia analalama kwenye mitandao huku lakini sidhani kama angekuwa ananipenda angekuwa ananisema vibaya kuwa mimi natumia unga yeye muache alalame mi nafanya yangu”
Lakini pia alizidi kwakusema kuwa alikuwa akifanya video ikabadilika na kuwa masinema.
Comments
comments