Msani Ommy Dimpoz amesahihisha mashabiki walipokuwa wakisema msanii huyo kafulia baada ya kukaa kimya muda mrefu kwenye game, na kusema aliamu tu kupumizka kwa muda na si kama alifulia.
Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Ommy Dimpoz amesema watanzania wamekuwa na mtazamo tofauti sana hasa pale msanii anapokuwa kimya kwenye kazi zake, na kukimbilia kumlaumu.
“Mimi nilikuwa kimya nilikuwa nafanya mambo yangu mengine, lakini sio kama kukaa kwangu kimya nilikuwa nimepotea nimepotea kwenye muziki, unajua watanzania wamekuwa na tafsiri tofauti, kuna watu wanatake break kija Justin Timberlake wanakaa miaka 7 7, na mimi nilikuwa zangu vacation, ma Ibiza huko (Ibiza ni sehemu ambayo watu wenye mkwanja mrefu duniani ndio huenda kula bata), sasa nimerudi nataka kufanya kazi”, alisema Ommy Dimpoz.
Ommy Dimpoz ambaye amerudi na ngoma mpya ya Kajiandae ambayo amefanya na Alikiba na tayari ameshaachia video yake, imepata ushabiki mkubwa mitandaoni kutokana na video yake.
eatv.tv
Comments
comments