-->

Nimepata Pakufia- Shilole

Msanii Shilole ‘Shishi Trump’ amefunguka kwa kudai yupo katika maandalizi yake ya mwisho ya kuolewa huku akiwasisitizia mashabiki zake kuwa safari hii hakuna maneno mengi kama zamani kwa kuwa amepata haja ya moyo wake.


Shilole amebainisha hayo baada ya baadhi ya mashabiki zake kutomuamini kwa kauli zake kwa kuwa mara nyingi ameonekana kuwa mwenye ‘drama’ nyingi katika mambo ya msingi anayowataarifu watu.
“Nipo kwenye maandalizi mazuri ya ndoa yangu lakini safari hii hakuna tena longo longo kama ambavyo ‘sometimes’ watu walivyozoea blah blah maneno mengi lakini mwanzo nilikuwa sijapata mahali pakufia lakini sasa hivi nimepata inabidi tu nikubali kufa”, alisema Shilole.
Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kwa kusema “Mungu akiamua kukuletea vitu vyake, anakuletea tu pale ambapo wewe hukutegemea wala kuwaza kama utapata. Unabaki kusema ‘realy’ hivyo haya yote ni mipango ya Mungu”.
Kwa upande mwingine, Shilole amebainisha kuwa chanzo cha kukutana na mume wake mtarajiwa ni katika sherehe ya msanii Linah Sanga ya ‘birthday’ iliyofanyikia mjini Zanzibar na ndiyo hapo mapenzi mubashara yakaanza mpaka leo.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364