-->

Nisha Adaiwa Kutapeli, Ang’aka!

Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kutapeli watu kwa dawa zake za kupunguza tumbo ambapo watu wamedai kuwa dawa hizo hazipunguzi chochote kama anavyozisifia.

nisha33

Salma Jabu ‘Nisha’

Kwa nyakati tofauti, watu wamemtolea Nisha malalamiko wakidai kuwa dawa anazozitangaza hazifanyi lolote bali anazitumia kuwachukulia watu fedha zao.

“Kiukweli mimi nimetumia dawa zake wala sijaona zikifanya lolote. Namuonya aache kwani atakuja kuingia kwenye kashfa,” alilalamika mmoja wa wateja aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.

Baada ya kupata malalamiko hayo, Wikienda lilimsaka Nisha ambapo alifunguka kuwa huo ni uzushi na anachoamini umeenezwa na watu wanaotaka kumuharibia biashara yake kwani hajawahi kupokea malalamiko yoyote.
“Wanaosema hivyo wana chuki binafsi na wivu, unajua kuna watu wakiona mtu anafanya biashara yake basi kazi yao ni kuwaharibia wenzao,” alisema Nisha.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364