MSANII wa Filamu hapa nchini, Salma Jabu ’Nisha’ amekuwa Balozi wa Kikundi cha New Hope Family Group chenye makazi yake Kigamboni Dar kinachojihusisha na masuala ya kutetea watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Hafla ya kumtambulisha msanii huyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambapo mwenyekiti wa taasisi hiyo, Omary Kombe, amesema lengo kubwa la kumteua Nisha kuwa balozi wao ni kutokana na mtazamo wao kuwa kupitia sanaa yake ya maigizo anaweza kuwa balozi mzuri kwani atatumia kipaji chake hicho katika kufikisha ujumbe kwenye jamii.
Amesema si tu kupitia sanaa 0yake, pia amejaaliwa kuwa na moyo wa upendo na huruma si tu kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi bali hata katika jamii ya watu maskini na wanyonge ambapo kwa kipindi cha miaka mingi wamekuwa wakiona na kusikia msanii huyo kutembelea vituo vya watoto waishio kwenye mazingira hatarishi huku akitoa misaada mbalimbali.
Kwa upande wake, Nisha amefurahi uteuzi huo kutokanana na kuonekana mchango wake kwenye jamii ambapo alisema atahakikisha anatumia sanaa yake vilivyo katika kutoa elimu juu ya watoto waishio katika mazingira magumu pamoja na kuiasa jamii kutambua kwamba inayo wajibu wa kuwapatia mahitaji ya msingi watoto waishio katika mazingira hatarishi.
(Na Denis Mtima/Gpl)
Mcheki hapa Nisha akiwa kwenye ubora wake ndani ya Kiboko Kabisa
Comments
comments