-->

Nisha Awatolea Uvivu Walioponda Shepu Yeka

Msanii wa filamu za kibongo Nisha bebe amewawakia mashabiki wanaomsema vibaya kwamba hana shepu, na kusema kuwa wasimlazimishe kuishi maisha feki.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Nisha ameandika ujumbe mrefu akionyesha kushangazwa na watu hao, huku akisema kwamba kuwa na shepu kwake sio kitu cha msingi, la muhimu ni akili ambazo amepewa na Mungu.

“Halafu nyinyi mnaosema nimepigwa pasi sijui sina shepu mnikome, tukivaa vigodoro maneno, mtu akiwa alivyo maneno, hemu chunguzeni wanawake wazuri wote duniani na wenye mashepu na status zao, ndiyo wale wanaoishia kupiga picha za uchi, kujiuza, kuishi kwa kutegemea mabwana na kadhalika. Omba Mungu akupe akili, afya njema, imani, heshima, upendo, maarifa na kipato, sote tumeumbwa kwa mfano wake”, aliandika Nisha bebe.

Nisha aliendelea kusema kwamba kama ni shepu uwezo wa kuweka shepu ya bandia anao, lakini hataki kumkufuru Mungu na kuamua kujikubali jinsi alivyo.

“Kutengeneza shepu ni dola 6000 tu (Milioni 10 na kadhaa) ni sawa na nisimamishe kusafiri safari mbili za nje ninazoenda kila ndani ya miezi miwili, nijibadili kwa kujitengeneza hizo shepu zenu India au Thailand. Napenda Mungu alichonipa na najivunia, siishi kifeki feki kama wewe borodozwa, we unayekosoa watu wakati huna mbele wala nyuma sura kama ulotapikwa na kobra, muda huo unaokosoa ungejiingizia kipato usingekuwa unakopa bando, najikubali na hali yangu.

 

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364