MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuhusu duka lake la nguo lililopo Sinza Makaburini, Dar kuvunjwa huku wengine wakihisi kavunjiwa kwa sababu za bomoabomoa jambo ambalo mwenyewe amesema si la kweli bali anafanya ukarabati.
Kuvunjwa kwa duka la Nisha kulizua sintofahamu kwa mashabiki wake hivi karibuni, jambo ambalo Show Biz Xtra ilimtafuta na kuzungumza naye ambapo alifunguka:
“Ni kweli eneo la duka langu lilibomolewa lakini si na manispaa kwa maana ya bomoabomoa kama wengi wanavyosema bali ni suala la marekebisho, soon nitakuwa hewani kama kawa,”alisema Nisha
Chanzo:GPL
Comments
comments