Nisha: Watoto Wamenitoa Machozi
Msanii wa filamu Tanzania Nisha ametoa sadaka kwa kufuturisha watoto wasiojiweza katika viwanja vya shule ya sekondari Azania Upanga Jumapili hii, futari iliyohudhuriwa na wasanii wenzake pamoja na watu kutoka sehemu mbalimbali.
Hata hivyo Nisha alipata wakati mgumu baada ya watoto hao kuanza kulia naye alishindwa kuvumilia huku akisema anawaonea huruma watoto hao na kuhisi kama ni yeye, hali iliyopelekea hata ‘kampani’ ya watu waliomsindikiza Nisha kulia pia.
Nisha amewaomba wadau mbalimbali nchini kujitolea na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kuweza kuwakwamua watoto hawa kwani wengine wanaweza kuwa na nyazifa mbalimbali hapo baadaye.
eatv.tv