Niva atambia kimombo
MWIGIZAJI Mohammed Zubery ‘Niva’, amefichua kuwa kujifunza kwake lugha ya Kiingereza kumemfungulia njia kwani sasa safari za kutoka na kwenda nje ya nchi zinajitokeza na hana hofu tena katika suala la mawasiliano na watu mbalimbali.
“Nawaambia kabisa, kila siku wasanii wenzangu wajifunze lugha tofauti, kwani nimesoma kozi ya Kiingereza na imeanza kujibu bwana safari zimeanza na sina hofu
tena ya mawasiliano. Nimeenda Rwanda kisha nitasepa Ulaya,” alisema Niva.
Niva alisema kuna umuhimu kwa msanii kujifunza Kiingereza kwani kwa kufanya hivyo kunampatia nafasi ya kuweza kushiriki katika usaili wa filamu nje ya nchi,
hivyo wigo wa msanii kufika mbali kimataifa katika masuala ya uigizaji na kutengeneza kipato zaidi, pia alidai wasanii Bongo wanakubalika sana Rwanda.