Niva Atembelea Watoto Wenye Shida Katika Kituo cha Taifa Kurasini
MWIGIZAJI wa kiume wa filamu Zuber Mohamed ‘Niva’ aka Super Mario leo hii mchana ametembelea kituo cha watoto wenye shida wanaoishi katika kituo cha Taifa kilichopo Kurasini katika Wilaya ya Temeke na kuweza kutoa zawadi kwa watoto hao ambao wapo pia watoto wenye matatizo mbalimbali na mtindio wa Ubongo.
Afisa Ustawi wa jamii ambaye ni mlezi wa kituo hicho Jack Omary ameshukru kwa msanii huyo kuweza kufika katika kituo hicho na kufurahi na watoto hao kwa kuwakumbuka na kuwapatia zawadi kama chakula sabuni, sukari, na vitu vingine kama shukrani yake na zawadi baada ya kufanikisha kufanya filamu ya Kasanga naye Mwana.
“Kwa niaba ya kituo chetu napenda kuwashukru sana kuja kututembelea na kutoa zawadi kwa watoto wetu ambao wana mahitaji mengi na tunaishukru Serikali kwani ndi mlezi mkuu wa kituo chetu chenye watoto 75, wakiwemo wa Chekechea, Shule ya Msingi na Sekondari pia,”anasema Jack.
Naye Niva amesema kuwa anajisikia furaha kwa kujumuika na watoto hao ambao wengi wao ni Yatima na wasio na wazazi wote wala ndugu wa karibu ambao wanaweza kubeba majukumu yanayowakabili kila siku iendayo kwa Mungu.
“Nimefurahi kuwa na watoto ambao wengi tumeambiwa kuwa ni Yatima hawana Baba wala mama jambo ambalo linahitaji kupata msaada hata wa kimawazo tu kutoka kwa wadau mbalimbali hata kula nao ni kitu kikubwa sana asanteni sana,”anasema Niva .
Niva anatarajia kuzunguka na kuongea na wapenzi wa kazi zake ikiwa ni katika kampeni ya kuongela filamu yake mpya inayojulikanakwa jina la Kasanga Naye Mwana ambayo inatarajia kutoka siku ya Jumatatu wiki ijayo tarehe 22/ February/ 2016. Kama mdau wa filamu USIIKOSE KASANGA NAYE MWANA Filamu ya Kitanzania.
FC