Klabu ya Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Young Africans (Yanga) yamwagikwa machozi baada ya Nahodha wao raia wa Rwanda Haruna Niyonzima kushindwa kufikia makubaliano ya kuendelea kuchezea klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake mwezi julai.
Hayo yamebainishwa na uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Katibu Mkuu, Boniface Mkwasa kwa kusema hawataweza kuendelea na Niyonzima katika msimu ujao wa 2017/2018 baada ya kumaliza mkataba wake mwezi Julai.
“Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga SC, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo, Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla” alisema Mkwasa
Niyonzima mbaye alichezea misimu sita mfululizo kwa kiwango cha juu bado haijawekwa wazi ni wapi anaelekea baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga SC.
eatv.tv
Comments
comments