Nuh Mziwanda Awalilia Mashabiki Wake
‘STRESS’ za kumwagana na aliyekuwa mke wake ambaye pia ni mzazi mwenziye, zinaendelea kuutesa ubongo wa mwanamuziki wa Bongo fleva, Nuh Mziwanda, ambapo hivi karibuni ameamua kuomba ushauri kwa mashabiki wake, juu ya mwanamke gani atamfaa katika maisha yake.
Nuh ambaye ni baba wa mtoto mmoja aliyezaa na aliyekuwa mkewe, Nawal, akiwa kwa sasa ni mke wa mwanaume mwingine anayeitwa Masoud, ametumia mtandao wa kijamii wa Instagram, kuwaomba ushauri mashabiki wake.
“Nimejifunza mengi sana kwenye ‘life style’ yangu ya kimapenzi na najitoaga sana, ila siku ya mwisho naumizwa, je unahisi mwanamke wa aina gani atanifaa na nitaweza kudumu naye? Leo nawaachieni mashabiki wangu mmalize hili,” ameandika Nuh.