Artists News in Tanzania

Nuh Mziwanda: Shilole Alikuwa Ananioteza, Hakupenda Nifanikiwe

Nuh Mziwanda amedai kuwa Shilole hakuwa mwanamke aliyekuwa akimshauri mambo ya msingi.

Akiongea na Clouds FM, Nuh amedai kuwa ex wake huyo hakuwa hata kumshauri ajijenge kimaisha kwakuwa alipenda aendelee kuwa tegemezi.

“Nilikuwa naishi kwa mwanamke wangu (Shilole) alikuwa hataki ninunue hata feni, hajawahi kuniambia ninunue friji,kitanda niweke nyumbani kwa mama yangu vikae,ila wazazi wangu na ndugu zangu walikuwa wakinihimiza kuwa umri unaenda nifungue akili yangu nifikirie ninachopaswa kufanya, mapenzi yasiniendekeze,” alisema muimbaji huyo.

Amesema pamoja na hayo mapenzi yalimfanya asione kama anapotea lakini amegundua walipoachana. Anasema ndugu zake walimshauri kuwa Shilole ni msichana mwenye maisha yake tayari na kwamba ana uwezo wa kumwacha muda wowote lakini hakusikia.

“Nimeyaona pia namwomba msamaha mama yangu,ndugu zangu,marafiki zangu waliokuwa wananipa ushauri mimi nilikuwa naona nimepata kuwa nimepatikana sasa hivi ni Nuh mpya nina maisha yangu ,nafanya shughuli zangu, alisisitiza.

Amedai kwa sasa amebadilika na ameanza kuishi kwake mwenyewe na kwamba kama asingekuwa na Shilole angekuwa mbali kwakuwa ex wake huyo hakupenda afanikiwe.


Mrembo mpya wa Nuh Mziwanda

Muimbaji huyo hivi karibuni alimuonesha yule anayeonekana kuwa mpenzi wake mpya. Shilole pia amekuwa akimuonesha mpenzi wake wa sasa ambaye pia ni msanii chipukizi, Nedy Music.


Shilole akiwa na mpenzi wake mpya, Nedy Music

Chanzo: Bongo5

Comments

comments

Exit mobile version