KUTOKANA na ugumu wa soko la filamu nchini lililosababisha wasambazaji wengi kuachana na kazi hiyo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ atauza kazi zake mwenyewe.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Odama alisema mara tu baada ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ataanza kusambaza kazi yake mpya aliyofanya hivi karibuni kwani kwa ugumu wa sasa sokoni, hawezi kumpa mtu amuuzie kama ilivyokuwa zamani.
“Kuanzia sasa nitauza filamu zangu nitakazocheza mwenyewe maana hali ya soko ni mbaya na ukisema kupeleka kwa wasambazaji naona nitapata hasara tu, ni bora niuze mwenyewe naamini nitauza sana kwa kuwa natengeneza filamu bora,” alisema Odama.
Chanzo:GPL
Comments
comments