Artists News in Tanzania

Ommy Dimpoz Afunguka Kutolipwa Alipokuwa Top Band

Msanii Ommy Dimpoz amesema kuwa alikuwa halipwi kitu alipokuwa Top Band, ommy  ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kusema kuwa hajayajutia magumu hayo, kwani alikuwa anajifunza.

OMMY21

“Mwanzo wakati naanza nipo Top Band nilikuwa siko vizuri financially (kifedha), nilikuwa sina hela, nilikuwa naenda kwenye shoo kwenye bendi, ilikuwa some times (wakati mwingine) tunapata, unajua nilikuwa najifunza kama unaenda gereji, unaweza ukaitengeneza gari yote mwenye fundi anakuelekeza alafu hela yote anachukua, lakini kama unaelewa hapa nipo najifunza utaona kawaida utasema hapa nipo najifunza”, alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz kwa sasa anamiliki lebo yake na kampuni yake ya Poz kwa Poz (PKP), na ameanza kwa kusaidia kuibua wasanii wachanga akiwemo Nedy Music, kitu ambacho alinukuliwa akisema kilikuwa ndoto yake ya siku nyingi.

eatv.tv

Comments

comments

Exit mobile version