Artists News in Tanzania

Pacha’ wa Harmonize Aangua Kilio Stejini

HARMORAPA, msanii chipukizi wa Bongo Fleva anayefanana sana kwa sura na msanii kutoka WCB, Harmonize kiasi cha kubatizwa jina la ‘Pacha wa Harmonize’, juzikati aliangua kilio stejini baada ya kukutana kwa mara nyingine na mkali huyo wa Ngoma za Matatizo, Aiyola na Bado, baada ya kupita muda mrefu bila kuonana.

Tukio hilo ‘ameizing’ lilijiri juzikati kwenye Ukumbi wa Maisha Basement, Kijitonyama jijini Dar ambapo Harmonize aliongozana na Dully Sykes na Queen Darleen katika kupiga shoo ya kuufungua mwaka mpya.

Katika kile ambacho Harmonize hakukitegemea, wakati anaingia ukumbini hapo, Harmorapa alikuwa ametega getini kwa shauku ya kumuona ambapo alipofika, jamaa alitumia kila njia akitaka kuzungumza naye bila mafanikio, kutokana na kuzuiliwa na mabaunsa.

Wakati shoo ikielekea ukingoni ndani ya ukumbi huo ambapo Harmonize alikuwa stejini, Harmorapa aliamua kujiongeza, akavamia jukwaa na kumkumbatia ‘pacha’ wake huyo huku machozi yakimtoka, jambo lililoamsha shangwe ukumbini hapo.

Tofauti na Harmonize anayeimba, msanii huyo chipukizi anarap na kuonesha jinsi anavyomhusudu Harmonize na jinsi anavyotaka kufanana naye kusiishie kwenye sura tu, ameamua kugandamizia mpaka jina lakini akabadilisha kidogo, kutoka Harmonize mpaka Harmorapa! Kweli duniani wawili wawili!

Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version