Wimbo wa Roma Waibua Maswali

SIKU mbili baada ya kuanza kusambaa mitandaoni na kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya redio, wimbo wa Msanii wa Bongo Fleva, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’, umeibua maswali mengi. Maswali yanaanzia kwenye jina la wimbo huo aliouita ‘Zimbabwe’, ambapo kwenye mashairi yake anasema ‘nakwenda Zimbabwe’, ambapo wengi wamejiuliza kwanini wimbo wa kuelezea kutekwa kwake aupe jina kama […]
Read More..Bill Gates Ajiunga Instagram Akiwa Tanzania...

Dar es Salaam. Tajiri namba moja duniani Bill Gates amejiunga Instagram akiwa nchini Tanzania na kurusha picha tatu ikiwemo aliyopiga na watoto akiwa Muheza mkoani Tanga. Gates ameijunga na mtandao huo wa kijamiii kwa jina la thisisbillgates na kurusha picha zake za kwanza tatu zote akiwa Tanzania. Gates katika mtandao huo aliandika hiki, “Hello kutoka Tanzania, […]
Read More..Mke Wangu Ameolewa Kabla Sijampa Talaka –...

Msanii wa muziki, Nuh Mziwanda amedai Baby Mama wake, Nawal alishinikizwa kuolewa na wazazi wake kabla hata ajampatia talaka. Muimbaji huyo amedai ingawa tayari aliyekuwa mke wake huyo ameshaolewa mtu mwingine lakini bado hajampatia talaka ya kusema kwamba wameachana. “Mimi sijaachana na Nawal, mpaka sasa mimi sijatoa talaka kusema mimi wewe sikutaki endelea na maisha […]
Read More..Sikuwahi Kujua Roma ni Msanii-Mke wa Roma (...

Mke wa msanii Roma Mkatoliki amefunguka na kusema kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na Roma Mkatoliki kwenye sherehe za kumnio na kudai msanii huyo alitambulisha kama Ibrahim na kusema kipindi hicho hakujua kama Roma ni msanii. Mke wa Roma Mkatoliki Nancy amesema hayo jana kupitia kipindi cha Friday Night Live (FLN) na kusema alikuja […]
Read More..Soma Magazeti ya Leo August 12 Hapa

Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 12 2017 kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa. Chanzo:Millardayo.com
Read More..Mke wa Roma Afungukia Roma Kuchepuka

Mke wa msanii Roma ameelezea jinsi mahusiano yake ya ndoa na rapper huyo yalivyo na kudai kuwa tabia ya wanaume kuchepuka kwenye ndoa ni wote wanayo. Baby Mama (Nancy) huyo ambaye alifunga ndoa na Roma mwaka 2015 ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa ni vigumu kujua kinachoendelea nyuma ya pazia kwa mwanaume ila kutokana na […]
Read More..Ney wa Mitego Sawa na Amber Lulu – Du...

Msanii Dudu Baya amemkingia kifua msanii Godzilla ambaye hivi karibuni amekuwa akiandamwa sana na msanii Ney wa Mitego akisema muziki umemshinda, na kumtaka Ney kutojifananisha na Godzilla. Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East AFrica Radio, Dudu Baya amesema Ney wa Mitego asithubutu kujifananisha na Godzilla kwani hawezi kufikia uwezo wa kuchana kama […]
Read More..DPP Aamua Kuachana na Mbunge Lwakatare Kuhu...

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameaondoa maombi yake dhidi ya Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare kuhusiana na shtaka la ugaidi dhidi yake. DPP alikuwa amefungua maombi Mahakama ya Rufani akiomba kibali cha kufungua maombi ya mapitio kuhusiana na uamuzi wa Mahakama Kuu kumfutia Lwakatare mashtaka ya ugaidi. Maombi hayo ya DPP […]
Read More..CUF Yapata Pigo Jingine

Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kmepata pigo jingine kufuatia Mahakama Kuu nchini Tanzania kutupilia mbali pingamizi lao kutaka Profesa Ibrahim Lipumba asipewe ruzuku za chama hicho. Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi hilo leo tarehe 11 Agosti 2017, kufuatia Chama Cha CUF huko nyuma kufungua kesi ya […]
Read More..Stara Thomas Atoboa Kinachowaharibu Wasanii...

Msanii mkongwe wa muziki Stara Thomas ameelezea sababu ya wasanii wengi wa kike wa sasa hivi kuimba nyimbo ambazo hazina maudhui na kupoteza ubora wa muziki, tofauti na ule ambao walikuwa wanafanya kipindi chao. Akizungumza kwenye kipidi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Stara Thomas amesema wasanii wa sasa hivi wanaimba muziki usio na […]
Read More..Ebitoke Afungukia Tetesi za Kubwagwa na Ben...

Mchekeshaji Ebitoke amedai si kweli penzi lake na Ben Pol limekufa bali wanafanya mambo yao kwa usiri zaidi. “Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani, hatutaki tuviweke hadharani. Hamna siyo vya unyago na siwezi kumuongelea vibaya Bentoke labda watu wanaona haniposti mimi kila siku lakini si hivyo,” ameiambia Times Fm. […]
Read More..NASA Wataka Odinga Atangazwe Rais

Muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, umeitaka Tume ya Uchaguzi nchini humo kumtangaza mgombea wake Raila Odinga kuwa mshindi wa Uchaguzi wa urais. Mmoja wa kiongozi wa muungano huo Musalia Mudavadi amesema wana ushahidi kutoka ndani ya Tume ya Uchaguzi kuwa, Odinga amepata kura Milioni 8, huku mpinzani wake rais Uhuru Kenyatta akipata kura Milioni […]
Read More..Siku ya Kucheza Muziki wa Nyumbani Yatafutw...

Dar es Salaam. Serikali imesema itafanya mazungumzo na viongozi wa muziki kujadili kuwa na siku maalumu ya muziki wa nyumbani. Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waimbaji wa muziki wa injili ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukutana na vikundi mbalimbali vya sanaa. Amesema […]
Read More..Alikiba ni wa Dhahabu – Mkubwa Fella

Meneja wa wasanii ambaye pia ni kiongozi wa kituo cha Mkubwa na wanawe Mkubwa Fella, amesema yeye hana tofauti na msanii yeyote, na kudai anaweza kufanya kazi hata na Alikiba ambaye wengi wanadhani ana tofauti naye kubwa. Mkubwa Fella ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Afrika Radio, na kusema kuwa hajawahi kugombana na Alikiba […]
Read More..IKULU: Rais Magufuli Akutana na Bill Gates....

Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kumshukuru Mwenyekiti Mwenza wa taasisi ya Bill and Mellinda Gates Bw. Bill Gates kwa misaada mbalimbali ambayo inatolewa kupitia taasisi yake kwenye miradi mbalimbali nchini.
Read More..Majambazi 13 Wauawa Kibiti, Wakutwa na Bund...

Jeshi la Polisi Tanzania limesema wahalifu 13 wameuawa katika majibizano ya risasi katika eneo la Tangibovu lililopo katika kijiji cha Miwaleni Tarafa ya Kibiti mkoani Pwani ambapo polisi wamefanikiwa kukamata bunduki 8, pikipiki 2 na begi la nguo. Jeshi la Polisi limeendeleza jitihada zake kuhakikisha mkoa wa Pwani na maeneo yake ya jirani yanakuwa salama […]
Read More..