Mwanamuziki wa rhumba nchini DRC Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kwa jina la Papa Wemba amefariki dunia leo nchini Ivory Coast.
Papaa Wemba amefariki dunia baada ya kuugua ghafla akiwa katika shughuli za kimuziki ambapo alianguka ghafla jukwaani katika tamasha la Festival des Musiques Urbaines d’Anoumabo (FEMUA) linaloendelea Abidjan, Ivory Coast.
Bado chanzo cha kifo hicho akijafahamika, na uchunguzi unaendelea.
Amefariki akiwa na umri wa miaka 66 amezaliwa Lubefu katika wilaya ya Sankuru Juni 14 mwaka 1949 nchini DRC wakati ikiitwa Congo ya Ubeligiji. (Belgian Congo)
Amewahi kufanya kazi za muziki na bendi mbalimbali nchini DRC zikiwemo Zaiko Langa Langa, Viva la Musica n.k
Papa Wemba atakumbukwa kwa nyimbo zake kama “Yolele”, “Kaukokokorobo”, “Show Me” pia kwa kupenda kutumia Kiswahili katika tungo zake.
eatv.tv
Comments
comments