-->

Pesa Zamfukuza Saida Karoli Kwenye Muziki

Mkongwe wa muziki wa asili wenye ladha ya bongo fleva, Saida Karoli amefunguka na kusema kwamba ukosefu wa pesa na mapromota waongo ndicho kitu pekee kilichomfanya apotee katika ramani ya muziki nchini.

Saida Karoli

Saida amefunguka hayo baada ya ujio wake mpya kwa kuachia  video inayokwenda kwa jina la ‘Orugambo’  na kuongeza kwamba aliamua kurudi kijijini kwao baada ya kukosa muelekeo maalumu.

“Nisingeweza kufanya kitu chochote bila kuwa na pesa, mapromota waliniangusha sana kipindi kile kitu ambacho kilinifanya nipotee. Sasa hivi nimerudi nashukuru Mungu japo sijapata uongozi lakini kuna watu wameamua kujitolea ili kipaji changu kisipotee”, Saida alifunguka

Kuhusiana na suala la kutengeneza muziki mzuri, Saida amesema muziki wake unaonekana kuwa mzuri  kwa sababu anatumia vitu vya asili katika kuutengeza .

“Muziki wangu mimi siandiki kabisa mashairi kwenye karatasi, huwa natunga mashairi wakati nikiwa studio napiga ngoma za asili. Huwa sipendi vionjo vya ngoma vinavyotengenezwa na kompyuta, na hiyo ndiyo sababu muziki wangu unakuwa na ladha ya tofauti”‘ Saida alizidi kufunguka.

Saida amewahi ametamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo, Maria Salome, Kizunguzungu na nyinginezo nyingi.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364