Artists News in Tanzania

Picha: Alikiba Atua Afrika Kusini Kwenye Tuzo za MTV MAMA

Staa wa Bongo Fleva, Alikiba ametua nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki kwenye utoaji tuzo za MTV MAMA akiwa na kiongozi wake wa Rockstar4000, Seven Mosha, meneja wake anayetambulika kwa jina la Aidan pamoja na Barakah The Prince.

Alikiba ni miongoni kati ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tuzo hizo Jumamosi hii ya Oktoba 22 mjini Johannesburg, Afrika Kusini lakini pia anawania tuzo ya ‘Best Collaboration’ ya wimbo wa Unconditionally Bae alioshirikiana na Sauti Sol. Tazama baadhi ya picha hapa chini.

 

Bongo5

 

Comments

comments

Exit mobile version