Picha: Umati Uliojitokeza Kuaga Miili ya Watoto Arusha
ARUSHA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan amewaongoza maelfu ya waombolezaji waliofika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha na Watanzania wote kuaga miili ya watoto waliofariki kwa ajali ya gari juzi Jumamosi.
Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.