Polisi Wadaiwa Kuuawa kwa Risasi Kibiti
Ikwiriri. Polisi saba waliokuwa doria katika Kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, wanadaiwa kuuawa usiku huu kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, lakini akasema taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani.
Taarifa za uhakika zilizolifikia Mwananchi Digital zimeeleza kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.
Chanzo:Mwananchi