-->

Pombe Ina Madhara Kuliko Bangi – Afande Sele

AFANDE34

Msanii mkongwe wa hip hop nchini, Afande Sele amefunguka na kusema serikali ihalalishe matumizi ya bangi na si kukosoa juu ya hoja iliyotolewa na mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma.

Ikiwa imepita siku moja toka mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM), kusema haoni sababu ya serikali kuzuia bangi kuwa zao la biashara kwa maana haoni madhara yake huku akidai kwamba viroba vina madhara zaidi kuliko bangi, Afande Sele amefunguka na kusema serikali ihalalishe matumizi ya bangi na si kukosoa juu ya hoja hiyo ya Joseph Msukuma.

Afande Sele amedai kuwa kuna nchi ambazo tayari wao wamehalalisha matumizi ya bangi na kuthibitisha kuwa pombe ina madhara makubwa zaidi kuliko bangi.

“Legalize it, Don’t criticize it. Korea, Kaskazini, Marekani, Mexico Uruguay na mataifa mengine ya Ulaya yamethibitisha pombe ina madhara kuliko Cannabis Sativa” Alisema Afande Sele.

Eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364