Baada ya kufungiwa Miezi 6 kutoa nyimbo mpya, kutumbuiza na kujihusisha na muziki kivyovyote, leo January 24 , 2018 Msanii Pretty Kind amesema sio kweli kwamba amefulia mpaka amekua akihongwa Elfu 20.
Pretty Kind alieleza kuwa washaabiki walichukulia vibaya alichosema kuhusu “WANANUME HAWAJUI KUHONGA”. Lakini aliomba msamaha kuhusu jambo hilo na pia kuahidi kubadilika.
Alisema kuwa kwa sasa ametulia na anataka akirudi aonesha kuwa amebadilika, sio tu kwenye mziki na kujihusisha pia mambo mengine kama biashara na kukaa karibu na jamii. Alikiri kusumbuliwa na wanaume na wengine kuchukulia matatizo yake kutaka kufanya mambo wanayotaka wao. Na kusema kuwa haishi kwa kumtegemea mwanaume.
Pretty kind pia alitoa pongezi kwa GIGI MONEY kwa kuweza kufungua biashara yake ya MAKEUP.
Na pia mwishoni Pretty kind alikiri kukubali makosa yake na kuomba tu wamsamehe kabisa au hata kumpunguzia adhabu aliopewa.
Comments
comments